Ticker

6/recent/ticker-posts

Waliokuwa Wakuu wa Mikoa Wanajeshi Wapandishwa vyeoRais Samia Suluhu Hassan amesema waliokuwa wakuu wa mikoa (Meja Jenerali Charles Mbuge na Brigedia Jenerali Marco Gaguti) wamerejea jeshini ambako kwa sasa wanahitajika na kwamba ameshawapandisha vyeo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Magogoni, Rais Samia amesema “kuna wakuu wa mikoa 26 hata hivyo nafasi zilizokuwa wazi ni 9 baada ya wakuu wa mikoa ambao walikuwa ni wanajeshi kuhitajika jeshini.”

Na kuongeza kuwa, “na jana niliwapandisha vyeo kuwa Meja Jenerali au Jenerali.”

Rais Samia Suluhu Hassan amesema viongozi hao wanaenda kutumikia Jeshi na amewachukua makanali wawili waliokuwa wakuu wa wilaya kuwa wakuu wa mikoa.

Kwa mujibu wa Rais Samia, nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa wilaya zitajazwa na wanajeshi (Makanali) wengine.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments