Yanga Yapigwa Faini ya Shilingi Milioni Moja na Laki Tano (1,500,000) Ligi Kuu Bara

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Klabu ya Soka ya Yanga, imepigwa faini ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) baada ya kukutwa na hatia ya kufanya makosa mawili.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeeleza kuwa Yanga imekutwa na makosa ya mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani katika mchezo kati yake na Polisi Tanzania uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Agosti 16, 2022.

Kosa lingine la Yanga kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa mikupuo minne badala ya mikupuo mitatu, kosa lililofanyika katika mechi kati ya timu hiyo na Coastal Union uliopigwa Agosti 20, 2022 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad