Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona SIMBA vs KMC..Simba hawakuwa na mechi nzuri"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



1: DAKIKA 90 za Presha kubwa. Dakika 90 za Israel na Roho ya Binadamu. Dakika 90 za Ushindani wa mwili na akili, KILA TIMU IMEPATA ALAMA ILIYOSTAHILI.

2: Simba hawakuwa na mechi nzuri sana! Ni kama Seleman Matola alikuwa na maamuzi mengi asiyoyaamini. Inatokea pindi kocha anapokuwa ‘caretaker’. Huna vipindi vya kutosha kwenye uwanja wa mazoezi kupanga Plan zako. Kivipi?

3: Simba walianza na umbo la 4-3-3, Kapama na Kanoute wakicheza nyuma ya Chama. Tusisahau hii ni mara ya kwanza Utatu huu kucheza pamoja kwenye mechi ya Ushindani. Mtego ulikuwa ni kumiliki mchezo na kushambulia kwa mapana ya uwanja

4: Tabu ikaja kwenye mfumo wa 4-4-2 Diamond waliyokuja nayo KMC! wakawa na idadi kubwa ya watu katikati ya uwanja! Ikawapa shida utatu wa Simba kucheza! Simba walifunga bao lakini hawakuwa na Dakika 45 bora sana kiwanjani

5: Kipindi cha pili KMC walibadili kidogo tu kwenye mfumo wao. Sub ya Matteo kwa Saliboko. George Makanga na Matteo wakaingia vyema kwenye wawili wa juu kwa roles za ‘4-4-2 Diamond’

6: GEORGE MAKANGA🙌 What A Goal! Changamoto yake kubwa ni muendelezo tu. Dakika chache baadae baada ya kufanya tukio la kipekee, akainyima timu pasi nzuri ya kuimaliza mechi… Bado namdai zaidi ya Leo Makanga

7: Moses Phiri.. What A Goal✅ Super.. Yes kuna makosa ya safu ya ulinzi Lakini huezi kuacha kuzungumza Quality ya Phiri namna alivyoutunza ule mpira na kuchagua mahala sahihi pa kucheza

8: Sakho hakuwa kwenye mchezo! Okrah pia.. Ni kama Simba kila mmoja alicheza kwa uwezo wake na sio timu. Ikawagharimu sana kupoteza mipira mingi

9: WELL DONE REFA RAMADHAN KAYOKO NA WASAIDIZI WAKE 👏 Baada ya usiku wa lawama na malalamiko kwa Waamuzi, Kayoko bila presha, amekuja kusimama Katikati na kulituliza Jahazi! WHAT A PERFORMANCE ✅ Alikuwa makini, anajiamini na aliuweka mchezo kwenye utawala wake.

10: Well Done Kijiri.. Ibrahim Ame✅ Kazi nzuri pia kwa sub za Simba kwa Spirit yao waliyoipeta kiwanjani. Tempo ya mechi ilipanda sana

Nb: Ghafla tu, Mzungu kawa mtoto wa kambo 😀
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad