Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA vs MTIBWA...Mtibwa ya Leo ni Edo Kumwembe mwenye Bia mkononi"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
1: MABAO 3. POINTI 3. CLEAN SHEET YA KWANZA KWA DIARRA.. BAO LA KWANZA KWA AZIZ KI.. Na kubwa zaidi, Ni MECHI YA 41 KWENYE LIGI BILA KUFUNGWA.. Salute kwa YANGA 👏

2: Kwa Lugha rahisi ya kueleweka kwenye mkusanyiko wa wanasoka ni kuwa MTIBWA WALIINGIA KWENYE MFUMO. KILA NABI ALICHOKITARAJIA AMEKIKUTA JUU YA MEZA.. Kivipi?

3: Mechi 2 zilizopita, Mtibwa walianza mechi ya Viungo wawili katikati.. Pascal Kitenge na Balama Mapinduzi.. Angalau mechi zilizopita alikuwa anaanza na Nassoro Kiziwa.. Leo pembeni alianza na Kibabage na Mhesa.. Timu ikawa rahisi kupitika katikati

4: Ni kama kocha wa Mtibwa, Salum Mayanga alitaka kupata Faida ya ‘kukosa utulivu’ wa Mabeki wa Yanga kwa kuufungua mchezo na kutaka kupishana.. QUALITY ya YANGA katikati na Mbele ikamuumiza vibaya sana

5: Kosa lingine kwa Mtibwa, Timu haikujua inaanza kukabia wapi. Timu ilitawanyika sana. Sio bahati mbaya Mtibwa wameruhusu Bao kwenye kila mchezo.. Kufunguka vile mbele ya Yanga ni kujiwekea kitanzi shingoni

6: FISTON MAYELE.. WHAT A PLAYER. WHAT A GOAL.🙌 Sina ninaloweza kuwalaumu mabeki wa Mtibwa pale.. Ponera alikimbia haraka kucover eneo la Mwihambi.. Lakini KASI na UBORA YA MAYELE ulikuwa kwenye kiwango cha juu sana..

7: Mtibwa wamepoteza mchezo Lakini ILAMFYA amepata somo zuri la vitendo kutoka kwa Mayele.. Utulivu, Maamuzi sahihi ndio tofauti kati yab Straika hatari na wa kawaida. Usiache kupitia notes za leo Ilamfya🤝

8: Well Done Kibabage! Licha ya udogo wake wa Umri lakini uwanjani ndio alikuwa mchezaji mkubwa aliyevaa jezi ya Mtibwa.. Alipambana sana kuisukuma timu mbele kwa kuchukua Risk za kuipasua safu ya kiungo ya Yanga

9: Zawadi Mauya.. Yes, alikuwa jibu zuri kwa Mtibwa pindi Yanga wanapokosa mpira. Nidhamu ya eneo na kusoma njia za shambulizi la mpinzani.. Changamoto yake ni nini afanye kwa haraka anapopata mpira.. Ana mengi ya Kuboresha kutokea Leo

10: Well Done Farid Mussa👏 Makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga yanaleta maswali mengi kuelekea mechi za kimataifa! Bado Nabi ana jukumu la kufanya kwenye uwanja wa mazoezi.. Timu inafikika kirahisi sana

Nb: Mtibwa ya Leo ni Edo Kumwembe mwenye Bia mkononi

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad