Babu Tale "Naandaliwa Mke Mzuri"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Mhe Hamisi Taletale maarufu Babu Tale ambaye alifiwa na mzazi mwenzie mwaka 2020, amesema anaamini Mungu anamuandalia mke mzuri wa kuja kuwalea wanae.

Tale ame-share hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, pia akiweka wazi kufiwa na mzazi mwenzie mwingine miezi miwili iliyopita aliyepata nae mtoto mmoja wa kiume jina Zahid.

"Najua wengi wenu mtajiuliza huyu mwengine ni nani? Sababu hao watatu sura zao sio ngeni sana machoni mwenu. Huyo mgeni kwenu anaitwa ZAHID. Ni mwanangu pia kama ilivyo hao watatu. Huyu nae nimempoteza Mama yake miezi miwili iliyopita. Sina budi kumshukuru Mungu kwakila mtihani anaonipa kwa maana anaamini nitauweza.

"Siwezi tena kulia, zaidi nakuomba uendelee kunifungulia riziki kila uchwao. Na naamini unaniandalia Mama yao mpya (mke mzuri) wakuja kuwalea na kuwaongoza kwenye misingi mizuri ya kumjua Mungu. Allah Asante kwakila Jambo." - Unasomeka ujumbe wa Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad