Barbara Gonzalez, Karia na Nyamlani Wateuliwa CAF


Watanzania wanne wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye Kamati mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) pamoja na Kamati ya Fedha.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani ameteuliwa kwenye Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) huku Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ni Mjumbe katika Kamati ya Mashindano ya Klabu.

Aidha Katibu Mtendaii wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha ameteuliwa kuwa Mjumbe katika Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya CAF.


💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad