Bomu Lateguliwa Benki ya NMB Shinyanga

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha tukio la bomu kutelekezwa na mtu asiyejulikana katika benki ya NMB tawi la Shinyanga.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mtu huyo aliingia ndani ya benki hiyo kama mteja akiwa amebeba begi, na kwenda kulitelekeza katika moja ya meza zilizopo ndani ya benki hiyo.

Baada ya muda mfupi begi hilo lililotelekezwa lilionekana likitoa cheche za moto na ndipo mmoja wa watumishi katika benki hiyo ya NMB tawi la Shinyanga alijaribu kuzima cheche hizo bila ya mafanikio.

Ndipo mtumishi huyo aliomba msaada kwa vyombo vya ulinzi , ambavyo vilifanikiwa kulitegua bomu hilo na kulitoa nje ya eneo la benki.

Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) amezungumza kwa njia ya simu na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi ambaye amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa suala hilo lipo kiusalama zaidi.

“Labda nikuambie hili limekaa kiusalama zaidi limetokea siku nne zilizopita, sio tukio la jana ,leo wala juzi ila limekaa kiusalama zaidi ili kutotisha wananchi.” amesema Kamanda Magomi

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad