Diamond Platnumz Anatumia Milioni 6 Kila Mwezi Kusukwa - Msusi wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPALisma, ambaye ni msusi wa wasanii alisema Diamond huwa anatumia milioni 3 mara mbili kwa mwezi.
Mwanasalon asema Diamond anamlipa milioni 3 za Tanzania kumsuka
Blogi moja nchini Tanzania imeibua taarifa mpya kabisa kuhusu yule mtu ambaye anashughulika kutakatisha kichwa cha msanii namba moja wa muda wote Afrika Mashariki, Diamond Platnumz.

Inaarifiwa kwamba mitindo ya usukaji wa Diamond Platnumz ni kazi ya mikono ya mwanadada mmoja mwenye saluni maarufu kwa jina Lisma.

Diamond ni msanii ambaye mara kwa mara anaonekana kubadilisha mitindo ya ususi kichwani mwake na kazi hiyo hufanywa na mwanadada Lisma. Inasemekana Diamond hulipa kiasi cha milioni tatu za Tanzania sawa na laki moja na nusu pesa za Kenya kila mara anaposukwa na Lisma.

Katika mahojiano, Lisma alifichua kuwa msanii Diamond husuka mara mbili kwa mwezi na kila mara anapotembelea saluni yake basi huwa anaacha kima cha 154K pesa za Kenya kwa ajili tu ya kusukwa.


Mwanadada huyo si tu msusi wa msanii Diamond bali pia anawashughulikia mastaa mbali mbali, wake kwa waume nchini humo na kufanya mionekano ya vichwa vyao kuvutia kwa mashabiki.

Lisma ndiye msusi wa mastaa mbali mbali kama vile aliyekuwa mpenzi wa Diamond Wema Sepetu, aliyekuwa mpenzi wa Rayvanny, Fahyvanny, msanii wa kike ndani ya WCB Zuchu, miongoni mwa majina mengine tajika nchini humo.

Watu mbali mbali wamekuwa wakimsifia msanii Diamond Paltnumz kwamba si mchoyo katika kumwaga mihela. Chawa wake Issa Azam mara kadhaa amenukuliwa akimsifia pakubwa kwamba msanii huyo amebadilisha maisha ya watu wengi na hata akasikika akisema kwamab ikatokea amefariki dunia leo basi atakayemzika awe ni Platnumz na wala si ndugu zake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad