Harryson Mwakyembe Ashangazwa na Uingereza Kumfungia Bondia Mwakinyo


Waziri wa zamani wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harryson Mwakyembe amesema ameshtushwa na taarifa zilizosambaa za Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo kufungiwa kucheza ngumi nchini Uingereza kwa muda usiojulikana.

Kauli hii ya Dr. Mwakyembe imekuja baada ya Mtandao wa ngumi za kulipwa duniani (BOXREC) kuchapisha taarifa kwamba Bondia Mwakinyo amefungiwa na Bodi ya Ngumi za kulipwa Uingereza (BBBC) kushiriki pambano lolote Nchini humo.

Dr. Mwakyembe ameandika "Nimeshtushwa na taarifa hii ya Bondia wetu Mwakinyo kuchukuliwa hatua hiyo na BBBC, Kamisheni yetu ya Ndondi za kulipwa (PBRC) inasemaje kuhusu hili? ni kweli au ni porojo za kimtandao? kama ni kweli Kamisheni yetu imechukua hatua gani kujua sababu za hatua hiyo na kifanyike nini kumsaidia Kijana wetu ikiwa hakutendewa haki?"

Taarifa hiyo haikueleza chanzo cha Bondia huyo namba moja nchini kufungiwa ambapo hata hivyo kulingana na taratibu za ngumi za kulipwa, imeelezwa kuwa kufungiwa huko hakutoathiri yeye kucheza ngumi Nchi nyingine duniani.


💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad