Jela miaka 30 kwa kumpa mimba mwanae

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kiteto, imemhukumu kifungo cha miaka 30, Yerenia Chidaka, mkazi wa Kijiji cha Dongo wilayani humo, baada ya kuzini na kumtia mimba mtoto wake wa miaka 16.
Mtuhumiwa amekiri kosa hilo hii leo Septemba 7, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mosi Sasy, na kusema hataki kuisumbua Mahakama kwa kuwa aliamua kuzini na mtoto wake huyo hakutaka aolewe na kabila la Wakamba.

Aidha Baba huyo imeelezwa kuwa alipomuuliza mke wake juu ya suala la kutotaka mtoto wao aolewe na Wakamba, mkewe alimjibu kwa dhihaka kwamba kama hataki aolewe basi amuoe yeye na ndipo alipoamua kumpa ujauzito.

Alipotakiwa kujitetea, mtuhumiwa aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa shetani alimpitia kutenda kosa hilo,huku Mwendesha Mashtaka wa Polisi Mahakamani hapo Inspekta Wilfred Mollel, akisema Jeshi la Polisi halina taarifa kama mtuhumiwa aliwahi kufanya kosa zaidi ya hilo na kumwomba Hakimu kumpa adhabu inayostahiki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad