Kinda la Tanzania Limeanza Maisha Mapya Barcelona

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAKAMA ambavyo ilikuwa kwa mshambuliaji kinda wa Kitanzania, Kelvin John kuanza maisha yake ya soka kwenye kituo cha Brooke House FA huko Uingereza kwa ajili ya kuzoea maisha ya Ulaya kabla ya kutua KRC Genk ndivyo ambavyo inaweza kuwa kwa Barka Seif ambaye amejiunga na MARCET Football University ambayo alipita Ansu Fati akiwa mdogo kabla ya kuibukia Barcelona.


Julai mosi, 2021 baada ya kuonekana ameiva, Kelvin alijiunga rasmi na KRC Genk ya Ubelgiji ambayo ilionyesha kumhitaji angali akiwa na miaka 17 ambapo alikuwa akifanya vizuri na kikosi cha vijana cha timu ya taifa ‘Serengeti Boys’.


Akiwa na Brooke House FA, Kelvin alitajwa kuwa mmoja wa makinda ambayo yanaweza kufanya makubwa miaka ijayo, ni kama nyota njema alianza kuwaka mapema na hatimaye kwa sasa licha ya kuwa na miaka 19 anapambania namba kwenye kikosi cha kwanza cha KRC Genk akiwa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.


Inawezekana Barka licha ya kuwa na umri mdogo zaidi kuliko Kelvin wakati akiingia Ulaya akafuata nyayo za mshambuliaji huyo.


Kwanini? Wiki chache zilizopita Barka alikuwa Uholanzi ambako alienda kwa mara ya pili kwa ajili ya kliniki kwenye klabu ya Ajax ambayo imetoa wachezaji wengi wakubwa ambao kwa sasa wanafanya vizuri Ulaya, akiwa huko yametoka maelekezo ambapo anatakiwa kuanzia MARCET Football University.

MARCET Football University ikoje tutalitazama hilo baadaye. Nje ya Bongo ilifanya mawasiliano na baba wa kijana huyo, Seif Mpanda na hapa anaeleza kuwa tayari mwanaye ameanza maisha mapya nchini Hispania kwenye chuo hicho.


Chanzo: Mwanaspoti


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad