Kumekucha: Zanzibar Yalaani Kitendo Cha Watalii Wawili wa Jinsia ya Kiume Kuvishana Pete Ufukweni



Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kupitia Kamisheni ya Utalii Zanzibar imelaani kitendo cha Watalii wawili wa jinsia moja (Wanaume) kuvishana pete katika ufukwe wa Hoteli iliyopo Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja na kusema uchunguzi unaendelea na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote walioandaa, kusimamia na kuhusika na tukio hilo ambalo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Kizanzibari.

Taarifa iliyotolewa na Kamisheni ya Utalii imesomeka kama ifuatavyo “Mnamo September 20, 2022 Serikali ya Zanzibar ilipokea taarifa kuhusu tukio hilo baada ya video kusambazwa kwenye mitandao ya kijami, kilichotokea ni ukiukwaji wa sheria za Zanzibar, tunawahimiza Wawekezaji, Wadau na Wageni kutoshiriki kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha mmomonyoko wa maadili au kuvuruga amani katika Jamii zetu”

“Tunatoa onyo kwamba vitendo kama hivyo havitovumiliwa, kilichofanyika ni kinyume na sheria mbalimbali za Zanzibar ikiwemo sheria ya utalii ya Znz namba 6 ya mwaka 2009 kifungu cha 27 (2), tunaomba Wananchi wawe watulivu wakati Vyombo husika vikiendelea na hatua stahiki” imeeleza taarifa hiyo.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA



 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad