Mlinzi Agutuka Baada ya Rais Ruto Kujifungulia Mlango wa Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Kinyume na taratibu, Rais William Ruto alijjifungulia mlango wa gari lake mwenyewe, huku akimuacha mlinzi wake akigutuka ghafla bin vuu kwa kuchelewa.


Kwenye picha zilizotapakaa mitandaoni, Ruto anaonekana akiwasili kwenye ubalozi wa Uingereza huku akijifungulia mlango wa gari lake.

Wakati huo, mlinzi wake mkuu Brigadia Timothy Stelu Lekolool anaoenekana akisonga hara upesi ili kujifanyia mwenyewe ila alichelewa.


Majukumu ya mlinzi wa Rais ambaye ni afisa wa jeshi, ni kwamba anatakiwa kumfuata Rais kila anapokwenda kutekeleza majukumu yake rasmi.



Mlinzi huyo anapaswa kumsindikiza Rais akitoka Ikulu na kumsubiri kumfungulia mlango wa gari linalomngoja, na kupiga saluti wakati Rais anapoondoka kwenye gari.

Pia mlinzi huyo anapswa kumbebea Rais vifaa vyake kama vile simu na hotuba. Pia hupokea zawadi na vifaa vingine kwa niaba ya Rais.

Siku ya Jumatano, Rais alizuru ubalozi huo wa humu nchini, ambako alipokelewa na Balozi Jane Marriot, na kutia saini kitambo cha kutoa rambirambi kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth wa Uingereza.

Pia hufanya kazi kwa karibu na Kamanda wa 'Presidential Escort Unit', ambaye anasimamia ulinzi wa Rais na pia ya familia yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad