Mwamba Amuua Mwenzake na Tofali Baada ya Kumkumbatia Mkewe Wakicheza Mziki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Razalius Kufabasi (50) Mkazi wa Kijiji cha Lusala Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga na tofali la kuchoma Linus Mtega (52) na kumsababishia umauti kwa kosa la kumkumbatia Mke wake wakati wakicheza muziki.


Imeelezwa kuwa siku ya tukio kulikuwa na shughuli ya kujengea makaburi ambapo majira ya usiku Watu walikuwa wakiburudika kwa muziki hivyo Mtega alikuwa amemkumbatia Mke wa Kufabasi huku wakicheza pamoja kitu ambacho kilimpa wivu Kufabasi na kupelekea kuchukua tofali na kumpiga kwenye paji la uso .


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Mtega alichanika paji lake la uso na kupelekwa katika Kituo cha Afya cha Mlangali alikofikwa na umauti.


Kamanda Issah amelaani vikali tabia hizo huku akiitaka Jamii kuacha wivu uliopitiliza kwani yanapotokea mauaji kama hayo Familia pamoja na Watoto ndio huteseka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad