Mwigulu Atoa Majibu Kuhusu Tozo

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Waziri mwenye dhamana ya fedha, Mwigulu Nchemba amesema serikali imeyapokea maoni yote yaliyotolewa na wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu tozo na makato yaliyoongezwa kwenye miamala ya kibenki na mitandao ya simu.

Akijibu maswali ya wana habari leo jijini Dodoma, Mwigulu nchemba amenukuliwa akisema “Yote tumeyasikia na kuyapokea na ni maoni mazuri na yenye tija katika kujenga nchi. Sisi wote ni Watanzania na hakuna Mtanzania na nusu hivyo maoni yetu yanahitajika katika kuhakikisha tunaijenga Tanzania moja na serikali ipo tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi”.

Ameendelea kusema kuwa hili ni jambo la kitaifa na hivyo watu waache kuchukua nafasi hiyo kumshambulia yeye binafsi na kumchafua kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameagiza mabasi 60 kupitia pesa hizi za tozo na amesisitiza kuwa watu hao waache mara moja kwakuwa yeye nyumbani kwake anamabweni mawili yanayokaliwa na wananwake na wanaume katika juhudi anazofanya katika kusaidia wanafunzi kupata malazi na hivyo hamiliki kampuni yoyote ya mabasi, pikipiki na hata bajaji.


Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba
Mwigulu nchemba amenukuliwa pia akisema “Maendeleo yanaanza na maono ambayo baadae yanafanyiwa utekelezaji.Rais Samia anamaono na hizi tozo zitakuja kuifaidisha nchi hii na raia wake huko mbeleni, mbali na maumivu wanayopitia wanachi lakini huko mbeleni nchi na wanachi watafaidika nayo”.

Pia katika kujibu hoja ya kodi ya majengo kwa wapangaji ameeleza kuwa hilo wataliangalia na kulipatia majibu ili kuepuka kuzuka kwa ugomvi baina ya mwenye nyumba na mpangaji na pia amesisitiza kuwa kuna wamiliki wa nyumba wanaoingiza fedha nyingi kwa mwaka zaidi ya milioni 60 na wanataka kuwa na hali ya usawa katika ulipaji wa kodi ya jengo na mtu mwenye kipato cha chini ambacho ni milioni 3 kwa mwaka, jambo hili haliwezi kuwa sawa.

Imeandaliwa na Simon Molanga kwa msaada wa mtandao.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad