Mwimbaji Abby Chams Amlipua Zuchu

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAMwishoni mwa wikiendi iliyoisha @officialzuchu aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter, ujumbe ambao uliibua hisia za watu wengi hasa wanamuziki wenzake wakike ambapo ujumbe huo ulipata mapokeo tofauti tofauti huku kila MTU akiujibu anavyoona yeye.

Watu ambao walionesha kumjibu ni pamoja na Ruby, Maua Sama na Nandy huku wengine walionesha kuingolea tweet hiyo kwa njia tofauti. Sasa mapema wiki hii @abigail_chams nae alikuwa na mtazamo wake kuhusu tweet hiyo ya Zuchu ambapo yeye kwenye ujumbe wake ameonyesha moja kwa moja kutofurahishwa na sehemu ya ujumbe huo.

@abigail_chams amemjibu @officialzuchu kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kueleza kwamba, ameangushwa kusoma na kitu kama hicho kutoka kwa Zuchu yaani hajapenda Zuchu kusema kwamba hataki kufananishwa na wanawake wenzake. Yeye yupo katika LIGI ya wanaume.

@abigail_chams ameeleza kwamba Zuchu hapaswi kusema hivyo kwa sababu uandishi haujali kwamba huyu ni mwandishi wa kike na mwandishi wa kiume. Wote wana uwezo wa kuandika vizuri na wana vipaji sawa.

"Kwa kusema hivi una maanisha kwamba vipaji vya wanaume na kuandika ni vya uwezo mkubwa zaidi kuliko vya wanawake?" Amehoji @abigail_chams na kuendelea, "Sio mafanikio ya aina yoyote kuwa katika LIGI ya wanaume (yovyote vile ambavyo umemaanisha). Inategemea zaidi kipaji na uwezo wa mtu huyo. Mwandishi mwenye kipaji ni mwandishi mwenye kipaji, ndio hivyo, haihusiani na jinsia".

Ujumbe @abigail_chams umeendelea, "Tusitegemee jamii kuchukulia Wanawake kwa kutilia maanani katika tasnia ya muziki kama sisi wenyewe hatueshimu tunachokifanya."

✍️: @omaryramsey


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad