Polisi watoa kauli Kuzuiwa Kupita MwendokasiBaada ya video fupi kusambaa jana ikionesha Askari Polisi wakizozana na Walinzi/Wafanyakazi wa barabara ya Mabasi ya mwendokasi, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali na kusisitiza kuwa barabara hiyo ni kwa ajili ya Mabasi ya Mwendokasi tu na hakuna chombo kingine chochote kinatakiwa kuitumia.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime imesema barabara hiyo haitakiwi kutumiwa na chombo kingine chochote isipokuwa Mabasi ya mwendokasi pekee.

“Si kwa Raia wala kwa Mtu yeyote, mwenye cheo cha aina yoyote awe anaendesha mwenyewe au anaendeshwa anayeruhusiwa kupita katika Barabara za Mwendokasi”

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad