Queen Darleen "Kwasasa Naishi Maisha ya Furaha Baada ya Kuondoka Kwenye Ndoa"


Queen Darleen ameibuka kusema kwamba acha watu wamuone mjinga ila baada ya kuachana na ndoa na kuchukua njia yake kwasasa anaishi maisha yenye furaha kuliko wakati alipokuwa ameolewa

Queen Darleen amesema hayo wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya kusikitisha ya mwanamke wa Nigeria aliyefariki dunia wakati akikimbizana kwa gari na mume wake aliyekuwa na mchepuko ndani ya gari jingine, ambapo mwanamke husika ambaye alikuwa mwanasheria imeelezwa alikuwa anapitia manyanyaso ndani ya ndoa na pia mume husika alikuwa hajatulia anaendekeza umalaya na kutoheshimu misingi ya ndoa

Indaiwa pia kwasasa aliyekuwa mume wa Queen Darleen yupo na mwanamke mwingine ukiacha yule mke mkubwa ambaye walielezwa waliondoa tofauti zao za awali

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad