Rapa Cardi B kutoka Marekani Afunguka "Ni Muda wa Harusi Yangu Sasa"


Rapa Cardi B kutoka Marekani, ameweka wazi kuwa ni muda wa harusi yake sasa na mumewe rapa Kiari Kendrell Cephus maarufu kama Offset, baada ya kufikisha miaka mitano ya ndoa yao.

Fahamu, kwenye moja ya mahojiano ya rapa Cardi B mwaka 2019 alifunguka kuhusu harusi yake ambayo kwa mwaka huo aliahirisha kufanya, alikaririwa akisema, “Tutatumia fedha nyingi katika harusi yetu, sidhani kama ni sawa kumuacha Offset kulipa kila kitu, nahisi nitalipa zaidi yake kwani gauni langu huenda likagharimu dola 50,000.”

Cardi B na Mumewe Offset wamejaaliwa kupata watoto wawili, Kulture Kiari Cephus na Wave Set Cephus katika ndoa yao ambayo walifunga Septemba 20, mwaka 2017 huko Atlanta, Georgia.


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad