Sababu ya Rais William Ruto Kutolala Katika Ikulu ya Nairobi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Rais William Ruto bado hajahamia katika Ikulu licha ya mtangulizw wake, Uhuru Kenyatta kuondoka kwenye makao hayo rasmi ya kiongozi wa taifa
Inadaiwa kwamba Ruto alikuwa akitumia Ikulu kufanyia mikutano yake akiwa Rais, ila kuamua kurejea kwenye makao yake ya Karen kulala
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa Ruto aliamua kusalia Karen katika makao rasmi ya Naibu Rais, kwa sababu Ikulu kwa sasa inafanyiwa ukarabati kwa jinsi itakavyomfurahisha
Rais William Ruto bado hajahamia katika Ikulu ya Nairobi, licha ya mtangulizi wake Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuondoka kwenye makao hayo rasmi ya kiongozi wa taifa.

Sababu ya Rais William Ruto Kutolala Katika Ikulu ya Nairobi
Rais William Ruto akiwa Ikulu. Picha: UGC.
Inadaiwa kwamba Ruto alikuwa akitumia Ikulu kufanyia mikutano yake akiwa Rais, ila kuamua kurejea kwenye makao yake ya Karen kulala.

Duru za kuaminika zinaarifu kuwa Ruto aliamua kusalia eneo la Karen katika makao rasmi ya Naibu Rais, kwa sababu Ikulu kwa sasa inafanyiwa ukarabati kwa jinsi itakavyomfurahisha yeye.

Mabadiliko Aliyofanya Rais William Ruto Alipochukua Usukani Katika Ikulu
Ukarabati huo unatarajiwa kuchukua kipindi cha miezi mitatu hivi, ila hautaathiri kivyovyote utendakazi wake akiwa kiongozi wa nchi.


"Ukarabati wa Ikulu umeanza na huenda ukachukua miezi mitatu kabla ya Rais kuhamia pale, haswa upande wa kuishi. Kwa sasa, ataendelea kutumia ofisi za Ikulu huku akiishi Karen," mwandani wa karibu wa Ruto aliiambia jarida la the Standard.

Ruto alibadilisha samani za Ikulu, zikiwemo viti ambavyo vilivyokuwa vikitumika awali na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Vile vile alibadilisha akaunti za mitandao ya kijamii za Ikulu na kmuweka picha zinazohusishwa na uongozi wake mpya.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad