Sauti ya Rubani wa Ndege Iliyomuua Mchezaji Emiliano Sala Akienda Kujiunga na Cardiff City Yanaswa


Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, rubani wa ndege iliyokuwa imembeba mwanasoka wa Argentina Emiliano Sala aliwaambia rafiki zake kuwa ndege ile ilikuwa na matatizo kabla haijapata ajali.Emiliano Sala

Sauti ya rubani David Ibbotson (59) imesikika ikisema ”nitavaa jaketi langu la kujiokolea nikiwa kwenye safari kutoka Ufaransa kwenda Wales,”

”Mara ya mwisho kuendesha hii ndege kuna kishindo nilikisikia, halafu pedeli ya breki ya kushoto haifanyi kazi, hii ndege ingerudishwa kwenye banda ikakae.”

Ndege hiyo ilipata ajali mwaka 2019 wakati Sala akitokea Nantes kuelekea kujiunga na Cardiff City baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 15.

Ibbotson ambaye alifariki pamoja na Sala kwenye ajali hiyo alikuwa ni rubani asiye na leseni ya kuendesha abiria wanaolipa.

David Henderson , mfanyabiashara aliyehusika kuandaa safari hiyo bila kibali anatumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la kuweka usalama wa watu na ndege hatarini.

#KitengeUpdates

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad