Serikali: Hakuna atakayekamatwa kwa kukosa bima ya afya

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAWakati Serikali ikiwasilisha muswada wa Bima ya Afya kwa Wote bungeni, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hakuna mtu atakaye kamatwa au kupigwa faini kwa kutokuwa na bima ya afya.

  Waziri Ummy aliyabainisha hayo leo Jumanne Septemba 27 jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, akisema Serikali imependekeza bima ya afya kuwa lazima, lakini hakuna mwananchi atakayekamatwa.

"Hakuna Mtanzania atakayefungwa au kukamatwa kwa kutokuwa na bima ya afya, hakuna hicho kifungu. Lakini tunawapataje Watanzania ambao hawaumwi kujiunga na bima ya afya? Ndio maana tumefungamanisha bima ya afya na baadhi ya huduma,” amesema.

Amezitaja huduma hizo kuwa pamoja na leseni ya biashara na leseni ya udereva.

“Unawampata wapi Watanzani ambao hawaumwi inabdidi umsubiri kwenye kitambulisho na leseni ya udereva," amesema.

Amesema lengo la serikali kuja na bima ya afya kwa wote ni kuwapunguzia mzigo wananchi kwenye matibabu.

Advertisement Aidha ameongeza kuwa si lazima Watanzania wote wajiunge na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) kwani kutakuwa na wigo mpana wa wananchi kuchagua taasisi waitakayo.

"Kama vile bima ya gari, unataka kuwa na gari lako lazima uwe na bima, kwahiyo unaweza kuwa na binafsi au ya serikali.

“Kwenye muswada tunapendekeza kuwe na kitita cha mafao chenye usawa ambacho kila atakayejiunga na bima ya afya atakuwa na haki ya kupata," amesema.

Ummy amesema huduma ambazo zitapatikana kwa kila mwananchi kwenye bima ya afya kwa wote ni pamoja na CT scan, X Ray na Ultrasound.

Ameeleza kuwa Bunge litakapopotisha muswada huo wa bima ya afya kwa wote utekelezaji wa sheria hiyo utaanza Julai 2023.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad