Sita wafariki ajali ya gari Kiteto

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Kiteto. Watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chekanao wilayani Kiteto mkoani Manyara.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha ajali hiyo akisema gari hilo lilikuwa linatoka Matui kwenda Kondoa mkoani Dodoma.

Kamanda Katabazi amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Septemba 19 asubuhi.

Amesema gari hilo la abiria lilikuwa linatokea Matui wilayani Kiteto likielekea Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

"Gari hilo mini basi lililokuwa linatokea Matui lilipata ajali eneo la Chekanao kata ya Kiperesa wakati likielekea Wilayani Kondoa mkoani Dodoma" amesema Katabazi.

Amesema miili ya marehemu na majeruhi hao ipo kwenye hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad