Walioua Polisi Wahukumiwa Kunyongwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Tabora.  Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imewahukumu washtakiwa wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuua askari wawili wa Jeshi la Polisi Kituo cha Usoke, wilayani Urambo mkoani Tabora.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Septemba 16, 2022 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, aliyekasimiwa mamlaka ya ziada, Jovin Katto, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni Shedrack Hamis Rushikama, Sylvester Mussa Kingwendu, Abel Benedict na Ramadhani Kassim Manywele ambao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu Katto amesema mahakama hiyo pasipo shaka imewatia hatiani washtakiwa hao baada ya kupata ushahidi usiotia shaka.

Awali, upande wa mashtaka ukiongozwa na Mawakili Meroto Ukongoji na Tunosye Luketa, uliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo, Aprili 28, 2014 usiku eneo la Usoke.

Uliongeza kusema kwamba siku hiyo washtakiwa waliwaua Askari polisi wenye Namba G3388 PC Shabani Mbua na Namba G 4602 kwa kuwapiga risasi.

Askari hao wawili waliuawa wakati wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama kwenye kituo cha Polisi cha Ussoke wilayani Urambo mkoani Tabora mwaka 2014.

Akitoa uamuzi huo Hakimu aliyepewa mamlaka ya ziada, Jovin Katto amesema mahakama imewatia hatiani kwa makosa hayo hivyo inawahukumu kunyongwa hadi kufa lakini wanaruhusiwa kukata rufaa kama hawakuridhika na adhabu hiyo.

Upande wa utetezi katika shauri hilo ulikuwa unawakilishwa na mawakili Fravian Francis, Amos Gaise,  Christina Jackson na Charles Ayo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad