Wanaume Kuweni Makini, Sio Kila Page ya Pisi kali Instagram Inamilikiwa na Huyo Unayemuona


Wanaume wa Mikoani kuweni makini sana, sio kila page ya pisi kali inamilikiwa na huyo unayemuona Kwenye picha

Page nyingi za Pisi kali ni za Wanaume wa Hovyo. Wamekosa Mchongo Mjini wanaamua Kufungua account ya Kike, wanatafuta Picha za pisi fulani either ndani ya Tz au Nje then anajifanya ndio yeye na anaanza kupost.

Wengine wapo Smart, unakuta Wana followers wengi kuliko Mtu halisi, hivyo ukiwa wa Kuja unaweza ukajua Hiyo ndio Official, then unatupia Swaga zako, anakukubali unaanza kupigwa hela, unakuja kuzinduka Ushapigwa parefu mno.

Kuna watu nchi hii bado washamba sana, unakuta Kuna page inaitwa "Zuchuuu" ina followers 200k then Watu wana-comment Zuchu nakukubali, Ngoma Yako kali. Hivi Watu wa hivi huwa wanajielewa kweli? Unashindwa kutambua Account ya kweli ya Zuchu?

VIPI UMEWAHI TONGOZA PISI UKIJUA NI YENYEWE LAKINI MWISHO WA SIKU UKAGUNDUA NI MWANAUME?

By Hopetyga

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad