Watanzania 3 Wauwawa Nairobi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Watu watatu wamefariki katika ajali ya barabarani eneo la Loitoktok nchini Kenya baada ya pikipiki mbili kugongana.


Watatu hao walipoteza maisha baada ya kugongana ana kwa ana kwa pikipiki zao walizokuwa wakiendesha ambapo wawili waliaga dunia eneo la ajali huku abiria aliyekuwa amebebwa kwenye pikipiki moja akiaga dunia wakati akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Loitoktok.


Kamanda wa polisi wa Loitoktok Shadrack Ruto alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya Ijumaa, Septemba 16, 2022 majira ya saa mbili usiku.


Jina la Lukuvi lamkamatisha tapeli

“Waendeshaji wanashukiwa kuwa kwenye mwendo wa kasi sana walipogongana,” Ruto alisema.


Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, wahusika wanakisiwa kuwa raia wa taifa la Tanzania kwa kuwa nambari za usajili za pikipiki hizo ni za taifa hilo.


Ruto alihimiza uangalifu barabarani huku miili ya waliofariki ikipelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Loitoktok.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad