Bima ya Afya kwa wote kutumika hospitali zote

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa, Bima ya Afya kwa wote itatoa fursa kwa Mtanzania mwenye hali yoyote kwenda kupata matibabu hospitali yoyote ikiwemo Muhimbili na nyingine za kibingwa.

Prof. Makubi amesema hayo, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Mkoa ya Amana, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na waganga wafawidhi wa Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke, Tumbi, Mbagala Rangitatu, Kigamboni walioongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Rashid Mfaume

“Kumbukeni Bima ya Afya itakapopitishwa mgonjwa atakuwa na haki ya kutibiwa hospitali yoyote anayoitaka, yaweza kuwa hospitali ya binafsi au ya serikali, sasa niwakumbushe kujipanga vizuri katika kutoa huduma bora na kutatua kero za wananchi ikiwemo kukaa muda mrefu, matumizi ya lugha nzuri na misongamano isiyo ya lazima,” amesema Prof. Makubi.

Amesema wananchi wana haki ya kupatiwa huduma bora, hususan katika kipindi hiki, ambacho serikali imewekeza katika upatikanaji wa dawa, miundombinu bora, vifaa tiba pamoja na ongezeko la watumishi katika maeneo ya kutolea huduma za afya nchini.


Ameelekeza uongozi wa Hospitali kutoa mafunzo ya huduma kwa mteja, ikiwemo matumizi ya lugha nzuri na zenye staha kwa walinzi wa usalama wanaochaguliwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma, ili kuondoa malalamiko yanayoweza kuzuilika kutoka kwa wananchi.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad