Mtoto wa Rais Museveni Aiomba Msamaha Kenya, Anataka Kuzuru Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mtoto wa rais Yower Museveni wa Uganda, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametangaza kutembelea Tanzania, ikiwa ni siku chache tangu azue utata wa kuiteka Nairobi kwa wiki mbili.


Licha ya baba yake kuomba radhi kwa niaba yake na yeye mwenyewe kumuomba radhi Rais wa Kenya, William Ruto kupitia mtandao wa twitter, machapisho hayo yalizua hasira kwa wakenya na kuleta mjadala mkubwa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.


Mtoto huyo anasifika kwa kauli na machapisho ‘tata’ hasa kupitia mtandao wake wa twitter wenye wafuasi Zaidi ya 600,000. Moja ya machapisho yake yaliyozua gumzo ukiacha kuiteka Nairobi kwa wiki mbili ni pamoja na kutangaza kustaafu jeshi, kutaka kumposa mtoto Waziri mkuu wa Italia, kuliunga mkono jeshi la Tigray, TPLF


Baba yake alilazimika kumuondoa kwenye nafasi yake ya mkuu wa vikosi vya ardhini lakini akampandisha na kuwa jenerali kamili, akimuwekakaribu kama mshauri wake.


Kupitia mtandao wake wa twitter, Kainerugaba ameandika tena kutaka kutembelea Tanzania, akimsifu pia rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu kwa kuweka picha ya kiongozi huyo akiwa na magwanda ya jeshi.


Hajaeleza dhumuni la kutaka kuitembelea Tanzania. Lakini ujumbe wake huo umeanza kuzua mjadala, ingawa watanzania wengi walioandika kwenye ukurasa wake, wakionekana kumkaribisha.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad