google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mwanafunzi Ajiua kwa Kunywa Sumu ya Panya | UDAKU SPECIAL

Mwanafunzi Ajiua kwa Kunywa Sumu ya Panya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Geita. Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Nyabubere kata ya Kasamwa wilayani Geita, Janeth Charles amefariki dunia akidaiwa kunywa sumu ya panya.

Mganga Mfawidhi Zahanati ya Nyakahongora, Ndime Mgini amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema mwanafunzi huyo alifikishwa kituoni hapo Oktoba 24, 2022 akiwa anatapika na kuharisha.

Mgini amesema baada ya kumpokea mwanafunzi huyo walianza kumpa huduma ya kwanza lakini muda mfupi baadaye alifariki dunia.

Amesema wakati anapatiwa matibabu mwanafunzi huyo alisema kuwa amekunywa sumu ya panya na alipoulizwa sababu za kufanya hivyo hakujibu chochote.


Baba mzazi wa mtoto huyo, Charles Rugwesa amesema siku hiyo mwanaye hakwenda shule kutokana na nguo kutokauka na alishinda akiteka maji lakini saa saba mchana baada ya mama yake kuivisha chakula cha mchana aliitwa kwa ajili ya kula na alikula kidogo kisha kutoka nje.

“Mara ghafla akarudi na kuingia chumbani akajilaza kitandani akaanza kutapika na kuharisha akawa anapiga kelele akisema mama na kufa tulimbeba na kumpeleka zahanati wakaanza kumhudumia wakamuongezea maji mililini lakini baada ya dakika chache akafariki”alisema Rugwesa.

Katekista wa Kanisa Katoliki Nyakahongola, Richard Lucas akiongoza ibada ya mazishi ya mwanafunzi huyo amewataka wazazi kuwa karibu na watoto na kuishi nao kwa upendo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad