Zari Aibu Yake! Asutwa Kutembea na ‘Vitoto’ Wanae Wamkataa Kibenteni Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Penzi la mwanamama Zari The Boss Lady kwa mpenzi wake mdogo kiumri (kibenteni) aitwaye mpenzi wake mdogo Shakib Cham Lutaaya linadaiwa kumpeleka puta kiasi cha kumtia aibu kwenye mitandao ya kijamii, IJUMAA linaripoti.

Zari ambaye ni mama wa watoto watano, ana umri wa miaka 42; umri unaotajwa kuwa ni wa kina mama wengi wenye watoto wa zaidi ya miaka 20 ambao wanamshuhudia akifanya mambo ya ajabu kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu wanaomshuhudia Zari ambaye ni mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz wanajiuliza hivi haya anayoyafanya watoto wake huwa wanajisikiaj


ZARI AMEROGWA?

Wapo wanaokwenda mbali zaidi wakimsuta kutembea na ‘vitoto’ na kudai kuwa, si bure, huwenda mwanamama huyo raia wa Uganda labda amerogwa maana kwa akili ya kawaida mwanamke anayejitambua hawezi kupiga picha za utupu akishika na kufanyiwa vitendo vya chumbani na kijana mdogo mwenye umri sawa na mtoto wake wa kwanza, Pinto kisha kuziacha zisambae kwenye mitandao ya kijamii.

ZARI AJITETEA

Hata hivyo, baada ya kusemwa mno kuwa, anatia aibu, Zari amejitetea kwamba picha hizo zimesambaa kimakosa na anakusudia kuchukua hatua za kisheria.

Zari anasema kuwa, amefikia hatua ya kukatisha mkataba wake na hoteli moja ya kifahari ambapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake huyo kisha wakapiga picha hizo kwa ajili ya matangazo.


Zari anasema kuwa, amevunja mkataba wake na Hoteli ya Divine Resort & Spa iliyopo nchini Uganda baada ya mpigapicha mmoja wa hoteli hiyo kukiuka kifungu cha mkataba wao kilichosema kwamba picha na video zote zinapaswa kuidhinishwa naye kabla ya kuachiwa.

“Mpigapicha huyo ameweka picha za Zari kabla ya kuidhinishwa. Kuanzia sasa, Zari hatabanwa tena na mkataba huo na hata-tag Divine Resort and Spa kwenye posti zake zozote za mitandao ya kijamii,” sehemu ya barua ya kusitishwa kwa mkataba ambayo IJUMAA limeiona inasomeka.


Katika barua hiyo, Zari anatoa agizo kwa mpigapicha husika kufuta picha zake zote alizochapisha kwenye kurasa zake na zile ambazo alituma kwa watu kwa ajili ya kuzisambaza mitandaoni.

Pia aliizuia hoteli hiyo dhidi ya kutumia picha zake na mpenzi wake kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii au tovuti yao.


“Kukosa kuzingatia yaliyo hapo juu kutahitaji timu kuendelea na hatua za kisheria na fidia,” barua hiyo inasomeka.

Katika video aliyoposti huko Snapchat, Zari anadai kuwa, mpigapicha huyo alivunjisha picha hizo kwa sababu alitaka kuwa wa kwanza kutangaza habari za likizo yake na mpenzi wake kwenye tovuti yake.

Zari analalamikia hatua hiyo na kusema kuwa, mhusika alikosa weledi katika kazi yake na kukiuka makubaliano kati yake na hoteli.

“Baadhi ya picha hizo ni nzuri na nyingine kidogo ni mbaya,” anadokeza.

Picha kadhaa za Zari akijivinjari na mpenziwe mdogo zimekuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii kama moto wa kifuu.

ZARI MAUDHUI YA AIBU

Baadhi ya picha hizo haziwezi kuchapishwa kwenye gazeti kwani zinaonesha maudhui ya aibu ya kimapenzi.

Watu mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti juu ya picha hizo na uhusiano huo wa kimapenzi.


Penzi la Zari na Shakib lilianza kushamiri takriban miezi minne iliyopita; miezi michache tu baada ya Zari kutengana na mfanyibiashara wa Uganda aitwaye GK Choppa.


Cha kushangaza sasa ni kwamba, taarifa mpya zimeibuka kuwa Shakib amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Zari kwa takriba miaka minne.

Shakib mwenyewe, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Tiktok alifichua kuwa wamekuwa wakisukuma mapenzi yao kwa miaka kadhaa.


“Miaka minne pamoja….Wanandoa #Hadithiyamapenzi,” alisema chini ya video ya kumbukumbu zao pamoja.

Katika video hiyo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alionekana akiwa amemshika Zari walipokuwa wakiingia ndani ya klabu.

Kama maelezo yanayojitokeza ni ya kweli, basi inamaanisha Zari alikutana na Shakib mara baada ya kutengana na Diamond siku ile ya Februari 14, 2018 (Siku ya Wapendanao).


Zari na Diamond walikuwa wameishi pamoja kama wanandoa kwa miaka minne kabla ya kuachana mnamo Siku ya Wapendanao 2018.


Baada ya kutengana na staa huyo wa Bongo, Zari hata hivyo, amewahi kuonekana na mwanaume mwingine hata kabla ya uhusiano wake na Shakib

Inaaminika kuwa Zari alikuwa kwenye uhusiano na GK Choppa kwa miezi kadhaa kabla ya kutengana katika hali tatanishi.

Wakati wa uhusiano wao, Zari aliposti picha zake na Mganda huyo mara kwa mara.

Mwezi uliopita, Zari alidokeza kufunga pingu za maisha na Shakib baada ya kufichua kuwa mpenzi wake huyo wa sasa anapanga kupeleka posa kwa baba yake nchini Uganda.

“Shakib aliniambia kuwa anataka kukutana na baba yangu. Anataka kutoa posa kwa ajili ya ndoa, yuko tayari kunioa,” Zari alisema kwa Kiganda katika video ambayo ilipostiwa kwenye mtandao wa Snapchat.

ZARI AWATUPIA VIJEMBE WAKOSOAJI


Katika video hiyo fupi, Zari aliendelea kuwatupia vijembe wakosoaji wa penzi lake na Shakib huku akiwathibitishia kuwa juhudi zao za kuwatenganisha zilikuwa zimefeli.

“Waliosema itaishia kwa machozi rudini kwa waganga wenu mkaombe warudishe hela, uchawi haukufanya kazi,” alisema Zari.

Awali, Zari alikuwa amebainisha kuwa mpenzi wake huyo mpya amemletea amani ambayo imemwezesha kukua na kung’aa zaidi.

“Naanza kuwa mkubwa. Naona shavu. Nimejipa amani sana. Bwana Lutaaya (Shakib) unanipa amani sana kwa maana watu ngojeni niwaambie kuhusu amani ya akili, hiyo nawaambia hata ufanye nini, unakua mkubwa zaidi hata usipokula,” alisema Zari kupitia Tiktok.

Zari alimtaka Shakib kuendelea kumpatia mahaba anayompa na kumbainishia kuwa yanafanya kazi.

“Bwana Lutaaya chochote unachofanya, ongeza zaidi. Niongezee dozi nyingine, chochote unachofanya kwa sababu zinafanya kazi, zinafanya kazi. Hata hao wanaoroga wamekata tamaa, wanahitaji kurejeshewa pesa zao. Bado nina amani, nendeni mkaombe kurejeshewe pesa zenu,” alisema Zari.

Zari amekuwa akitetea uhusiano wake na Shakib hasa kwa kuwa amekosolewa sana kufuatia utofauti wao wa kiumri.

TIFFAH, NILLAN HAWAMTAKI SHAKIB

Katika ukosoaji huo, hata wanawe wawili wa mwisho wa Zari hawana upendo mkubwa kwa Shakib.

Tiffah Dangote na Prince Nillan ambazo Zari amezaa na Diamond wameonesha wazi kuwa hawako tayari mama yao kuchumbiana na Shakib katika kikao cha familia walichoagiza wakati baba yao, Diamond alipowatembelea Afrika Kusini hivi karibuni.

Katika kikao hicho, ndugu hao wawili walimlaumu mama yao kwa kuvunja uhusiano wake na Diamond miaka kadhaa iliyopita.


“Yeye (Zari) sasa yuko na mtu mwingine, nasema ukweli,” Tiffah Dangote alimwambia Diamond.

Huku akimuunga mkono dada yake, Prince Nillan alisema; “Kwa hivyo Mama T (Zari) ndiye aliyevunja familia.”

Diamond kwa utani aliyaunga mkono maoni ya watoto wake kwamba mpenzi wake huyo wa zamani  ndiye aliyevunja familia.

Ndugu hao wawili wenye umri wa miaka 7 na 5 walikanusha madai kuwa baba yao yuko katika uhusiano na mwanamke mwingine.

Pia walikana madai ya mama yao kuwa, Diamond ana watoto wengine kando yao.


“Siamini una mpenzi mwingine, siamini una watoto wengine,” alisema Tiffah.

Tiffah aliendelea kumlalamikia mama yake kwa kuvunja familia huku akimkosoa kwa kujitosa kwenye uhusiano na mwanaume mwingine.

Pia alimshtumu kwa kutumia muda wake mwingi na mpenzi wake huyo na kukosa muda wa kuwa na baba yao wampendaye.

“Kwa nini uliivunja familia? Uko na mtu mwingine, unatumia muda wako naye, huna wakati na familia, hatumii wakati wako na baba!” Tiffah alimlalamikia mama’ke.

Diamond ambaye alishangazwa na hisia za watoto wake alidokeza kuwa watakapokuja kubaini ukweli hatimaye watamshambulia.

Licha ya kufurahishwa na wanawe kwa kutomshtumu kwa kusababisha kuvunjika kwa familia, Diamond alimtetea Zari kwa watoto wao na kuwahakikishia kuwa familia bado ipo imara.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad