Afia kwenye nyumba ambayo haijakamilika

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Mtu mmoja mwanaume ambaye hakufahamika mara moja amekutwa amefariki katika nyumba moja inayoendelea na ujenzi wilayani Manyoni mkoani Singida, huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.
Imedaiwa kuwa huenda kifo hicho kimetokea siku kadhaa zilizopita kutokana na mwili huo kukutwa umeharibika.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini undani wa kifo hicho.

Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya wilaya Manyoni Dkt. Ainea Mlewa, amekiri kupokea mwili huo ambao umehifadhiwa katika chumba cha kuhidhia maiti.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad