Akamatwa kwa Kudanganya Polisi Ameporwa Mil. 60 Alitumwa na Boss wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Deodatus Thadei Luhela (35) kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kituo cha Polisi huku akidai kuwa majambazi walimjeruhi na kumpora Tsh Milioni 60,000,000 alizo kuwa ametumwa na mwajiri wake kuzichukua kutoka benki ya CRDB Tazara.


Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi kanda Maalum ya Dar es Saaam, ACP Jumanne Muliro ambapo amefafanua kuwa Mtuhumiwa huyo ambaye ni mhasibu wa Kampuni ya kichina iitwayo ‘‘your home Choice’’ iliyopo Keko alikamatwa Novemba 14, mwaka huu eneo la Chang’ombe Wilaya ya Temeke jijini Dar.


Baada ya tukio hilo majira ya saa 8 :00 mchana mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000, na makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walipomuhoji kwa kina na wakabaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo.


Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limemkamata Joseph James (32) mkazi wa Kijitonyama ambaye amekuwa akijifanya ni askari Polisi kutoka ofisi ya Upelelezi Makao Makuu ya Polisi Dodoma.


Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limeendelea kuwaonya watu weny nia ya kufanya vitendo vya uhalifu hasa mwishoni mwa mwaka kutofanya vitendo hivyo kwani Jeshi hilo lipo makini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad