Dk Mwakyembe akabidhi ripoti uchunguzi kufeli mawakili

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Dar es Salaam. Kamati ya kufuatilia mwenendo wa matokeo ya mitihani ya mafunzo ya uansheria kwa vitendo (LST), imeanisha changamoto nane ikisema ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Harrison Mwakyembe amesema changamoto hizo pia zimelalamikiwa na LST pamoja na wadau mbalimbali wa sheria.

Dk Mwakyembe ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 20, 2022 wakati akisoma muhtsari wa taarifa ya kamati hiyo kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani ya mafunzo katika taasisi ya LST.

Hafla hiyo imehudhuriwa  na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas  Ndumbaro, katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo,  wajumbe wa kamati hiyo pamoja viongozi waandamizi wa wizara hiyo.


Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, mwaka huu na Dk Ndumbaro na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo.

Sakata hilo lililoibuliwa na Mwananchi, lilitokana na matokeo ya awamu (Cohort) ya 35 ya wanafunzi wa taasisi hiyo, kuonyesha kati ya wanafunzi 633 waliofanya mtihani huo, ni 26 ndio waliofaulu kwa awamu ya kwanza.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 265 walifeli (discontinue) na wengine 242 walitakiwa kurudia mtihani (supplementary).


Akitoa taarifa hiyo leo, Dk Mwakyembe amesema udahili wa wanafunzi wengi kupita uwezo katika vyuo vinavyofundisha sheria na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo unasababisha uwiano mbaya kati walimu na wanafunzi na kuathiri ufundishaji na usimamizi.

Pia Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria  amesema kumekuwa na uhuria usio kuwa na tija kwa kila chuo kuwa na uhuru wa kupanga muda wa kukamilisha shahada ya sheria kati ya miaka mitatu au minne.

"Pia uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadaye kujiunga na LST katika kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza.Tatizo hili lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza," amesema Dk Mwakyembe.

Mbali na hilo, amesema uamuzi wa Tume ya Vyuo Vikuu kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita  kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili hadi alama nne ( D mbili kwa masomo mawili kulikowezessha vijana wasiokuwa na uwezo kusoma masomo ya sheria.


Dk Mwakyembe mbunge wa zamani wa Kyela mkoani Mbeya amesema utatuzi wa changamoto hizo upo kisera na kimfumo. Amesema mfumo wa bora wa elimuT ya sheria unasimamamiwa na ule uanasheria kwa vitendo unasimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria nchini (CLE).

Amesema kamati inashauri kufufuliwa kwa CLE na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kukaa chini na TCU kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria vyuo vikuu.

"Kuanzisha mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa wenzetu wa Afrika Mashariki ambao utasimamiwa na CLE, " amesema Dk Mwakyembe.

Dk Ndumbaro amesema, “leo tumepokea taarifa tunakwenda msituni, tutapitia changamoto kwa changamoto zilizoanishwa katika taarifa ya kamati hii” Dk Ndumbaro
mwananchi.co.tz
 Unmute


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad