Ticker

6/recent/ticker-posts

HAT TRICK yampa jeuri Mayele, afunguka mazito aliyopitia

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAMshambulaiji hatari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Kalala Mayele amefunguka na kueleza alivyokua anajihisi kwa kushinda kuifungia klabu hiyo kwa michezo kadhaa iliyopita.


Mayele alishindwa kuifungia Young Africans katika michezo mitano mfululizo iliyopita, hali ambayo iliibua taharuki kwa Mashabiki wake na wale ambao wanafuatilia Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.


Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo amesema alikua anajihisi vibaya kwa sababu jukumu lake kubwa ni kuisaidia timu kupata ushindi, na yeye amekua akitazamwa kama mkombozi kwa kuifungia Young Africans.

“Mimi kama Mshambuliaji huwa ninapambana kila mchezo niweze kufunga, ikitokea ninashindwa kufunga huwa sijihisi furaha kabisa, lakini nilikua ninaamini ipo siku nitafunga na leo (Jana) nimefanikiwa kufunga.” Amesema Mayele


Mayele alifunga mabao matatu pakee yake ‘HAT TRICK’, huku bao lingine likifungwa na Beki wa Kulia Shomari Kibwana na kuifanya Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

atua ya kuifungia Young Africans mabao matatu jana Alhamis (Novemba 17) dhidi Singida Big Stars inamuwezesha Meyele kufikisha mabao Sita msimu huu, sawa na Mshambuliaji wa Simba SC Moses Phiri, huku Sixtus Sabilo akiwa kileleni kwa kupachikwa mabao Saba.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments