KOCHA Alious Cisse wa Senegal Ajitwisha Mzigo "Lawama zote nipeni mimi Kufungwa Kombe la Dunia"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Baada ya kuanza vibaya Michuano ya Kombe la Dunia 2022, Kocha Mkuu wa Senegal Alious Cisse amesema anapaswa yeye kama Mkuu wa Benchi la Ufundi na sio wachezaji wake.


Senegal ipoteza mchezo wake wa kwanza wa Kundi A kwa kufungwa na Uholanzi Mabao 2-0 jana Jumatatu (Novemba 21), katika Uwanja wa Al Thumama, mjini Doha.


Cisse amesema Wachezaji wake hawapaswi kulaumuwa na yoyote aliyechukizwa na matokeo ya mchezo huo, badala yake lawama zote zielekezwe kwake kwa sababu alifanya maamuzi ya kila hatua walioipiga kwenye mchezo huo.


Amesema ikitokea Wachezaji wakaendelea kulaumiwa watakua wanakosewa sana, hivyo amesisitiza yeye kama Kocha Mkuu anapaswa lawama hizo na ikiwezekana akiulizwa ataweza kuzitolea ufafanuzi.


“Ninaweza kuwa mimi ndio mkosaji mkubwa kwa sababu mimi ndiye Kocha Mkuu. Ukishindwa lazima useme shida ni kocha. Mpira ni ufanisi, usipofunga huwezi kushinda.” amesema Cisse


Senegal iliweza kulinda isifungwe hadi dakika ya 83′ ya mchezo, lakini kwa bahati mbaya waliruhusu kupoteza kwa mabao ya Cody Math├Ęs Gakpo na Davy Klaassen yaliyofungwa dakika ya 84 na 90+ 9.

Ushindi wa Uholanzi unalifanya Kundi A kuwa na ushindani mkubwa kwani hadi sasa taifa hilo la Ulaya limefungana kwa alama na mabao ya kufunga na Ecuador, huku wenyeji QATAR na Senegal wakiburuza mkia wa Kundi hilo.Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad