Mhalifu Aliyeisumbua Sana FBI Mpaka Ikaamua Ifanye Naye Kazi tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mhalifu Aliyeisumbua Sana FBI Mpaka Ikaamua Ifanye Naye Kazi tu


🦅Kuna dogo alizaliwa April 27 ya mwaka 1948, anaitwa Frank William Abagnale.

🦅Huyu dogo bwana, alijua sana kuzihenyesha mamlaza za ulinzi na usalama za marekani vilivyo

🦅Inaaminika matukio yake mengi ya kihalifu, aliyatekeleza kipindi akiwa na kati ya miaka 16-21.

🦅Baadhi ya matukio aliyoyafanyaga katikati ya umri huo (16-21), ni pamoja na
1. Aliwahi kujitengenezea leseni feki ya udereva, na katika Leseni hio ilikua anaonesha kuwa alikua na Umri mara 10 zaidi ya umri aliokuwa nao kwa wakati huo.
2. Aliwahi kufungua accounts zake kadhaa za benki kwa kutumia taarifa za kibenki za watu wengine
3. Aliwahi kutengeneza Leseni feki ya urubani, kiasi kwamba alipata kazi ya urubani kwenye moja ya mashirika ya ndege huko New York.
4. Kipindi anafanya kazi ya Urubani, aliwahi Ku ghushi zaidi ya Dola za Kimarekani Milion 2.5
5. Baada ya Kuachana na kazi ya Urubani, alihamia kule Mjini Georgia ambapo alikwenda kujifanya ni mtaalamu wa masuala ya afya za watoto, ila hakudumu katika kazi hio baada ya siku moja kufanya ujinga ambao ungeweza kugharimu maisha ya mtoto mmoja aliyekuwa anamhudumia
6. Baada ya hapo, akaenda Kuomba kazi ya Uanasheria Katika kampuni moja huko Marekani, akidai kuwa alikuwa graduate degree yake ya sheria kutoka pale Harvard.

NB: Na Vyeti fake vya Harvard alikuwa navyo.

🦅Alikamatwa Mwaka 1969, na kutiwa gerezani. Lakini pindi akiwa gerezani akajifanya kuwa yeye ni askari kanzu wa polisi ambaye amekuja jela kwa ajili ya kupeleleza wafungwa, hivyo Gereza likawa linampa Special Treatments😂💔.

🦅Alikaa Jela kwa mda mfupi kisha akatoroka😂

Ila alikamatwa tena, ila mara hii FBI wakamchunguza sana kabla ya kutoa hukumu ya Moja Kwa Moja na hatimaye walibaini kuwa, dogo hakuwa na akili ya kawaida.

Kwasababu Matukio yote ambayo aliyafanya kama hilo la kuendesha Ndege,Kutibu Watoto n.k aliyafanya bila kufundishwa na mtu

Basi bwana, dogo akatolewa selo ila kwa sharti kuu kuwa “He must work for the FBI”.

Anatajwa kama “The most intelligent criminal in history”, yupo hai mpaka sasa na Anafanya kazi na FBI mpaka sasa.

Na huyo ndiye Frank William Abagnale jr.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad