Mwanamke Ajaribu Kufungua Mlango wa Ndege Ikiwa Angani Akidai Kuitwa na Yesu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Elom Agbegninou anashikiliwa na polisi kwa kujaribu kufungua mlango wa ndege ikiwa angani.

Tukio hilo limetokea Arkansas nchini Marekani ambapo mwanamke huyo akiwa ndani ya ndege, alianza kufanya fujo akitaka kufungua mlango wa ndege ikiwa angani, akidai alikuwa ameelekezwa na Yesu kufanya hivyo.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri na ndege ya Shirika la Southwest iliyokuwa ikitokea Houston, Texas kuelekea Columbus, Ohio ambapo taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea Jumamosi iliyopita.

Inaelezwa kuwa katika mtafaruku huo uliotokea ndege ikiwa umbali wa futi 37,000 kutoka usawa wa bahari, ambapo alipozuiwa kufanya kitendo hicho cha hatari, alimng'ata kidole mmoja wa watu waliokuwa wakimzuia.

Baada ya fujo kubwa ndani ya ndege, rubani alifanikiwa kutua kwa dharura kwenye Uwanja wa Ndege wa Bill and Hillary Clinton National Airport ambapo mwanamke huyo alitolewa na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad