Mwimbaji Jay Melody Apanic Baada ya Kupewa Makavu na Shabiki Kisa Kuimba Amapiano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Umekuwa ni muendelezo wa mastaa wa Bongo siku hizi kuwa na majibu makali kwa watu wanaocomment kwenye post zao hata kama Comments hizo ziko positive kwenye upande wa kushauri. Jay Melody amejikuta anapaniki baada ya shabiki wa muziki wake kumpa ushauri kuhusu wimbo wake mpya alioutoa aina ya Amapiano unaoitwa #achawivu

Shabiki huyo amemtaka Jay Melody kustick kwenye aina ya muziki ambao amekuwa akiufanya siku zote ambao umempatia hadi hits kadhaa kuliko kufanya amapiano ambazo si aina yake ya muziki na uwenda ni Marioo ndiye msanii pekee anaye upatia zaidi muziki huo. Jay Melody ameishia kutukana kwamba Amapiano yake sio Amapiano ya bwana ake na shabiki (Marioo), na uwa hapangiwi nini cha kufanya.

“Hii ni experience mpya so usipagawe, Amapiano kafanya Burna Boy, Diamond, Mbosso, Nandy, Damian Sol so huu sio mziki wa huyo bwana ako kwahiyo kaa kwa kutulia, pia hakuna mtu ananipangia wimbo wa kutoa hivo” Jay

Ifike hatua mastaa wa Bongo waache utoto kuona ni sifa kuwajibu watu hovyo na kutaka sifa za kinafiki, usifiwe wimbo mzuri, nyuma yako watu wanadiss. mtu anafuatilia kazi zako na ndiye huyo huyo ukiwa kwenye media unamtaka hasiache kukusupport, ifike hatua mastaa waache kuziona zaidi roho mbaya kwenye mawazo ya watu kuliko kuuona wema kwenye hayo mawazo, shabiki kashauri vizuri tu,jamaa anapaniki na kinacho muuma zaidi ni kuona msanii mwenzie ndiye kapendekezwa kwenye hiyo midundo, lazima akubali hawawezi fanana.

Jay Melody sikiliza watu, ushauri sio lazima uuchukue, bora uachane nao kimya kimya kuliko kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulivyo kwenye public, Hits Tatu zisikufanye ujione umeikamilisha safari, shabiki ana nia njema na wewe kuona unatengeneza utawala wako.🚮


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad