Ticker

6/recent/ticker-posts

Peter Msechu Afunguka Magumu Aliyopitia Mpaka Kumiliki Hii Nyumba Kali

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Nilipoamua kuwa na familia na kuishi kama baba nilijiwekea Malengo ya kuhakikisha naipa Furaha na Amani Familia yangu kwa namna yeyote ile.
Kuanzia Mwaka 2009 mara tu baada ya kumalizika Shindano la Bss Mimi na Mke wangu Mama lolo tulifanya maamuzi ambayo yalikuwa hayavumiliki wala kuwezekana kwani Tulipitia magumu na yasiyoelezeka tulipokubaliana kuanza kusave asilimia 50 ya kila pesa nitakayoingiza kwenye kazi yeyote ile ili tuweze kujenga. Haikuwa rahisi kwani kuna muda ilifika niligombana sana na Mama lolo kwani alikuwa akitaka kujua kila hela ninayopata na alidai na kuhakikisha ile asilimia 50 tuliyokubaliana inatengwa na haitumiki kwa vyovyote vile.

Tuligombana tulifokeana tulikwanzana tukanuniana ila leo hii Mimi na Mke wangu Mama lolo watoto wetu watatu Lauren, Lian na Levin Kwa furaha kubwa Tunapenda Kuwakaribisha Nyumbani kwetu 🏡🙏


Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments