Polisi feki akamatwa Dar

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Polisi feki akamatwa Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linafuatilia kundi la Watu waojifanya ni Askari Polisi wakati mwingine Maafisa wa Usalama wa Taifa ambao hukamata Watu hovyo, kuzunguka nao mitaani kwa kutumia gari huku wakiwatishia juu ya tuhuma mbalimbali za uongo na baadae kuwataka watoe pesa ndio wawaachie.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema katika ufuatiliaji wa suala hilo amekamatwa Joseph James (32) Mkazi wa Kijitonyama ambaye amekuwa akijifanya ni Askari Polisi kutoka Ofisi ya Upelelezi Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

“Uchunguzi umebaini, Mtuhumiwa huyu amekuwa akishirikiana na wenzake ambao wamekuwa wakitumia gari aina ya Subaru lenye namba za usajili T 550 DST alilokamatwa nalo Mtuhumiwa huyo”

“Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaenedelea kuwasaka Wahalifu wote wanaofanya utapeli wa namna hii ili wakamatwe na kufikishwa kwenye mifumo ya kisheria kwa hatua zaidi.”


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad