Rais Jacob Zuma Kurejea Gerezani Afrika Kusini

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Kufungwa kwake kulisababisha maandamano ya ghasia katika jimbo la KwaZulu Natal na maeneo mengine ya Afrika Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300
Kufungwa kwake kulisababisha maandamano ya ghasia katika jimbo la KwaZulu Natal na maeneo mengine ya Afrika Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300

Mahakama ya Juu ya Rufaa ya Afrika Kusini imeamuru Rais wa zamani Jacob Zuma kurejea gerezani baada ya kukubaliana na uamuzi wa awali kwamba ruhusa ya matibabu ilikuwa kinyume cha sheria.

Lakini haijabainika iwapo atarudi gerezani au la.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 alihukumiwa kifungo cha miezi 15 mwaka jana kwa kudharau mahakama kutokana na kukataa kutoa ushahidi wake wakati wa uchunguzi wa ufisadi.

Kufungwa kwake kulisababisha maandamano ya ghasia katika jimbo la KwaZulu Natal na maeneo mengine ya Afrika Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300.

Zuma aliachiliwa baada ya miezi miwili jela, baada ya mawakili wake kubainisha kuwa alikuwa na ugonjwa usiojulikana.

Katika uamuzi wao wa siku ya Jumatatu, majaji walisema kwamba mamlaka ya magereza inapaswa kuamua ikiwa muda ambao rais huyo wa zamani ametumia kinyume cha sheria nje ya jela unapaswa kuhesabiwa kuelekea kifungo chake au la.

Mawakili wa rais huyo wa zamani walikuwa wamedai kuwa Zuma alihitaji matibabu ambayo hayangeweza kutolewa gerezani na sasa anaweza kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Katiba.

Ni suala la kisheria lakini ambalo limekuwa na athari za kisiasa huko nyuma.

Kuna wasiwasi kwamba kurejea kwake gerezani kunaweza kusababisha kurudiwa kwa machafuko yaliyoonekana Julai.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad