Ronaldo kulipwa Bil 481/-Saudi Arabia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



CRISTIANO Ronaldo ameripotiwa kukubali mkataba wa mwaka mmoja unaovunja rekodi ya pauni milioni 172.9 sawa na shilingi bilioni 481.5 katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.

Mkataba wa Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 katika klabu ya Manchester United umevunjwa mapema mwezi huu kufuatia uhusuano wenye msukosuko na viongozi wa klabu na ulizidi kuwa mbaya alipotoa kauli zenye utata katika mahojiano na mtangazaji wa televisheni ya Talk, Piers Morgan.

Kwa mujibu wa gazeti la michezo, Marca la Hispania sasa Ronaldo anasemekana amekubali kihisia dili la miaka miwili na nusu katika klabu ya Al Nassr lenye thamani ya pauni milioni 172.9 kila mwaka litakalomwezesha acheze hadi kufikisha miaka 40.

Vyanzo vya habari vya karibu na nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus vimesisitiza kuwa hakuna saini iliyotiwa na kwamba Ronaldo ameweka maanani michuano ya Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Ureno.

Wakati wa majira ya joto Ronaldo alikuwa akishinikiza kuondoka Old Trafford lakini hakufanikiwa nia yake ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Al-Nassr ni moja ya timu zenye mafanikiwa zaidi Saudi Arabia ikiwa imebeba ubingwa wa nchi hiyo mara 9 na taji la Super Cup misimu ya 2020 na 2021.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad