Tite: Neymar Yupo Fiti Na Atacheza Mchezo Unaofuata Mashabiki Ondoeni Shaka

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 


KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Brazil Tite amethibitisha kuwa nyota wa timu hiyo na klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa Neymar Da Silva Junior ataendelea kushiriki mashindano ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar na atakuwepo katika kikosi kitakachocheza mchezo unaofuatia kwenye kundi lake.

Tite amelazimika kuibuka na kutoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa nyita huyo anaweza asiendelee na mashindano hayo kufuatia majeraha aliyoyapata katika kifundo chake cha mguu kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya Timu ya Taifa ya Serbia.


“Msijari Neymar atacheza Kombe la Dunia. Ataendelea kucheza, mnaweza kuwa na uhakika na hilo. Kocha Tite aliwaambia Waandishi wa Habari.


Katika mchezo huo dhidi ya Serbia, Timu ya Taifa ya Brazil ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yote yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wa Totenham Hotspurs Richarlison.Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad