Yanga: Akili Zetu Zinafikiria Ubingwa Tu Kwenye kila Mashindano Tunayoshiriki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



UONGOZI wa Yanga SC, umeweka wazi kuwa, akili zao zinafikiria kupata mafanikio kwenye kila mashindano wanayoshiriki kwa kubeba ubingwa.


Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambapo walisepa nalo msimu uliopita kutoka mikononi mwa watani zao wa jadi Simba.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ally Kamwe ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga, alisema: “Kwenye mashindano ambayo tunashiriki yote akili zetu ni kuona tunashinda ubingwa, hilo lipo wazi.

“Hakuna namna, ushindani kwenye ligi ni mgumu na wachezaji wanalijua hilo, hivyo ambacho tunakifanya ni kupata matokeo mazuri, hilo litafanyika mpaka mwisho wa msimu.”

Baada ya kucheza mechi 8 za Ligi Kuu Bara, Yanga imefikisha pointi 20, ipo kileleni mwa msimamo kabla ya mechi za jana Jumatano.

Timu hiyo ambayo jana ilicheza dhidi ya Club Africain katika kuwania kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, msimu huu tayari imebeba Ngao ya Jamii kwa kuifunga Simba mabao 2-1.


STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad