Binti wa Kazi Amnyonga Bosi Wake Kwa Kanga, Akutwa na Pete za Dhahabu na Kadi za Benki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Binti wa kazi mwenye umri wa miaka 15 aliyefahamika kwa jina la Sarah Sahani, anatuhumiwa kumnyonga hadi kupoteza maisha bosi wake ambaye ni Mhadhili wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agoustino cha mkoani Mwanza, Hamida Musa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, amesema mtuhumiwa huyo amekutwa na vitambulisho mbalimbali ikiwemo kadi za Benki.

Kamanda Mutafungwa amesema binti huyo alimnyonga bosi wake kwa kutumia kanga na kusababisha kifo chake kisha kutokomea na vitu vya thamani ikiwemo pete, televisheni na kadi za benki.

Katika tukio hilo, watuhumiwa wengine wawili wamekamatwa ambao wanatajwa kushirikiana na binti huyo kutekeleza mauaji ya Mhadhili huyo, aliyekuwa akiishi eneo la Buzuruga jijini Mwanza
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad