Mwanamuziki Auponda Mziki wa Rap "Siku Hizi Sisikilizi Tena Mziki Huo"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamuziki na Gwiji wa Afrobeat Barani Afrika @wizkidayo siku ya leo amezua sito fahamu kwenye mitandao ya kijamii hii ni kufuatia Shiti zake kuhusu Muziki wa Hip Hop kuwa umekufa nchini Nigeria. wiki hii alipokuwa akifanya mahojiano na 10 Magazine ambapo Chapisho lake la kwanza limetoka siku ya Alhamis.

Wizkid alinukuwa akisifia ukuaji wa muziki wa Afrobeats Kimataifa huku akiuponda Muziki wa Rap nchini Nigeria Wizkid alisema kuwa ukiachana na Afrobeats, huwa hasikilizi aina nyingine ya Muziki hususa Rap kwa sababu nyimbo nyingi zinazo tengenezwa hua zinaboa sana.

Big wizzy aliongeza kwa kusema “niwe mkweli tu sisikilizi aina nyingine yoyote ya muziki tena. Muziki wa Rap, huo upuuzi unaniboa sana Muziki umechoka na Tayari umekufa. hawa rapper wanafanya kitu kile kile cha kipuuzi kwenye midundo ile ile na Midondoko ile ile.” Alisema Big Wizzy.

Unaambiwa skuizi Wizkidayo amekua Muongeaji sana kitu ambacho hapo awali alikuwa hayupo hivyo Kupitia ukurasa wake wa Snapchart alipigilia Msumali mwingine kwakusema kuwa Kwenye game ya Rap anawakubali @nasty_csa @sarkodie na @blacksherif_ kwa hapa Afrika, ila wengine wote wamepigika yani hawana kitu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad