Ticker

6/recent/ticker-posts

Alikamatwa na Madawa ya Kulevya, Akatakiwa Kupigana Vita ya Ukraine na Urusi

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Kuhusu Mtanzania aliyefariki baada ya kujiunga kikosi cha kijeshi upande wa Urusi dhidi ya Ukraine

Taarifa za kifo cha Raia wa Tanzania, Nemes Tarimo, zilisambaa pamoja na video ikionesha akiwa anaagwa kwa heshima na vikosi vya jeshi nchini Urusi.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Tarimo, alikamatwa kwa kesi ya dawa za kulevya kisha akafungwa, baada ya muda alipatiwa taarifa za kujiunga na kundi la Wagner na kuahidiwa kuachiwa huru baada ya miezi sita ya kupambana katika uwanja wa vita.

‘’Alitupatia taarifa kuwa anajiunga kwenda kwenye vita dhidi ya Ukraine, tulimsihi sana asijiunge lakini akasema huwezi jua nitapata uhuru wangu kwa hiyo akajiunga na mara ya mwisho kuwasiliana ilikua Oktoba 17 na hakupatikana tena, ’’anasema ndugu wa Nemes ambaye hakutaka jina lake

Nemes alienda Urusi kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili katika Chuo cha Teknolojia cha Urusi, MIREA.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments