Ticker

6/recent/ticker-posts

Bodi ya Ligi Yasogeza Mbele Mechi Kariakoo Dabi Simba Dhidi ya Yanga

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAKiungo wa Simba Clatous Chama (katikati) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Yanga Azizi Ki (kushoto) na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ (kulia) katika moja ya mechi dabi ya Kariakoo.
BODI ya ligi Kuu Tanzania  TPLB, imetangaza mabadiliko ya tarehe ya michezo yote ya mzunguko  wa 26  ligi kuu ya NBC ikiwemo mechi ya Dabi kubwa nchini kati ya vilabu vya Kariakoo Simba na Yanga.

Dabi hiyo  sasa inatarajiwa kuchezwa Aprili 16, 2023 majira ya saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya Aprili 9, 2023.

Mabalidiko ya mchezo namba 184 mzunguko wa 23 utakaozikutanisha Simba na Yanga yametokana na kutolewa taarifa ya kutoka kwa wamiliki wa Uwanja wa Mkapa ikitaja uwepo wa mkutano wa dini Aprili 9, 2023 siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya mchezo huo.

Taarifa ya mabadiliko hayo ya tarehe yametangazwa rasmi na Bodi ya Ligi leo Januari 21, 2023.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments