Ticker

6/recent/ticker-posts

Ishu ya BM33, Aziz KI iko hivi

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA
YANGA inaendelea kujifua kwa ajili ya mechi yao ijayo dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting, huku kambi yao ikinoga baada ya kutua kwa nyota watatu waliokuwa hawajarejea kikosini winga Bernard Morrison, kiungo Stephane Aziz KI na beki Yannick Bangala, ambao hata hivyo wanasubiri kujua hatua watakazochukuliwa kwa kuchelewa.

Morrison alikuwa wa kwanza kurejea nchini kati ya hao, kisha akafuata Aziz KI na usiku wa kuamkia jana Bangala akakamilisha idadi yao lakini kuna jambo litawafuata nyuma baadhi yao.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba wawili kati ya hao wanaweza kukutana na adhabu ya kukatwa fedha kwa kuchelewa kujiunga na timu hiyo tangu.

Yanga ilirejea kazini Januari 10 na Mwanaspoti linafahamu kama wachezaji hao watashindwa kujitetea juu ya uchelewaji huo, huenda kila mchezaji akakatwa kiasi cha Sh100,000 kwenye mshahara wake kwa kila siku waliyokosa.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments