Ticker

6/recent/ticker-posts

Singida BS yaichapa Azam, mabao yaamua nafasi

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAMATOKEO ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata Singida Big Stars dhidi ya Azam FC, haujabadili chochote kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Licha ya SBS inafanana pointi 43 na Azam FC na michezo ya kushinda 13, sare nne,  lakini itasalia nafasi ya nne kwa utofauti wa mabao 12.
SBS imecheza mechi 21, imeshinda 13, sare nne na imefungwa michezo minne,inamiliki mabao 24, imetikiswa nyavuni mara 15 na ina pointi 43.
Azam FC imecheza mechi 21, imeshinda 13, sare nne, imefungwa mechi minne, ina mabao ya kufunga 36 mabao ya kufungwa 21 na ina pointi 43.

Singida Big Stars ilipata bao  dakika ya 45+ ambapo Bruno Gomes alipiga faulo nje ya boksi shuti lake likamshinda kipa wa Azam FC, Ali Ahamada.

Mzunguko wa kwanza Singida Big Stars, ilipoteza Uwanja wa Chamazi kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Sospeter Bajana dakika 47 akipokea pasi ya mwisho ya James Akaminko, hivyo hizo timu kila moja imeshinda kwenye uwanja wake.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments